Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Rais wa FIBA Africa Zone V Hesham EL Hariri, Rais wa TBF Phares Magesa na wachezaji wa timu ya vijana wa Under 18 wa Tanzania, katika ufungaji wa mashindano ya Basketball ya FIBA Zone V, uwanja wa ndani wa Taifa, Dar Es Salaam. Mhe. Waziri ametoa tuzo kwa washindi wote ambapo Rwanda wameshika nafasi 1 kwa Wasichana na Wavulana, Uganda nafasi ya 2 Wasichana na Wavulana na Tanzania nafasi ya 3 wasichana na wavulana.

Mhe. Waziri amewashukuru wadau wote walisaidia kufanikisha mashindano haya na amewatunuku vyeti vya shukurani, pia amezipongeza nchi zote zilizoshiriki na ameahidi kufanyia marekebisho makubwa uwanja wa ndani wa Taifa ili uwe na hadhi ya kimataifa, kabla ya mashindano yajayo ya Basketball ya FIBA Zone V Club Championship yatakayofanyika Tanzania 30 Sep-7Oct,2018.

Wadau wote tushirikiane kuendeleza kikapu Tanzania. For more info visit www.tbf.or.tz