Timu yetu ya Taifa ya 3×3  ijulikanayo kwa jina la WAZALENDO inatarajia kuondoka siku ya Ijumaa alfajiri 27 July 2018 kuelekea nchini Madagascar kwenda katika Mashindano ya 3×3 Africa Basketball Qualifiers 2018 ambayo yatashirikisha nchi 16 ambapo timu 4 kati hizo zitapata nafasi ya kushiriki Fainali za Africa, Afrobasket 3×3  zitakazofanyika nchini Togo, mwezi October, 2018.

Timu ya hii ya Tanzania inashirikisha baadhi ya wachezaji ambao walishiriki mashindano ya 3×3 FIBA Zone V U18 ambayo yalifanyika hapa Tanzania na timu yetu kuchukua nafasi ya pili na kufanikiwa kuingia mashindano ya Afro basket U18 yatayofanyika nchini Mali, baadae mwaka huu.

Wafuatao ndio watatuwakikisha Madagascar :

WACHEZAJI :

 1. ABBA PATRICK ROBERT
 2. HAJI RASHID MBEGU
 3. CHARLES ALBERT MAYOMBO
 4. RASHID TARIQ HAROUN MAARIFA
 5. JOVIN CHARLES NGOWE
 6. MWALIMU HERI KIJOGOO
 7. BARAKA NSAJI
 8. PHINIAS STEPHEN KASHABI
 9. JONAS MUSHI

VIONGOZI :

 1. KARABANI LAWRENCE KARABANI- Meneja wa timu na Mkuu wa Msafara
 2. ROBERT MNENDE MANYERERE – Kocha
 3. SHABANI MAHOBONYA – Afisa

Tunaishukuru Serikali, wazazi, makocha na  wadau wa kikapu mbali mbali ikiwemo kampuni ya FACTORY MEDIA PRODUCTION ambayo kwa sehemu kubwa imefanikisha safari hii, na wadau wengine ambao wameendelea kushirikiana nasi katika kuiandaa timu hii. Tunakaribisha wadau wengine na mashirika mbalimbali kuendelea kushirikiana nasi katika kuendeleza mchezo wa kikapu Tanzania.