Kituo cha vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK Park) kimezindua msimu mpya wa Jr.NBA leeague 2018. Uzinduzi ulifanywa rasmi na  Mr. Kita Matungulu (NBA Africa Basketball Operations Director) , Coach Bahati Mgunda (Jr NBA Program Manager) na Mr. Phares Magesa (Tanzania Basketball Federation President) ambaye alitoa nasaha zake wakati wa ufunguzi wa Ligi ya kikapu ya vijana wadogo (Junior NBA League) katika viwanja vya JMK.

Mashindano haya ni muhimu katika mpango wa maendeleo ya kikapu nchini na TBF imeahidi kuzidi kuyaimarisha na kuyaboresha mashindano mengi zaidi.

Jumla ya timu 60 na vijana 900 wanashariki mashindano haya, tunawashukuru NBA, Symbion, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Manispaa ya Ilala, Chama cha Basketball Mkoa wa DSM na wadau wote wanaosapoti Kikapu. Tunatarajia kuimarisha ushirikiano wetu na NBA na wadau wengine ili kuendeleza Kikapu, tushirikiane wote kujenga viwanja zaidi na kuhakikisha National Basketball League(NBL), Taifa Cup, FIBA Zone V U18 Nations Cup & Club Championships mwaka huu yanafanyika kwa mafanikio makubwa hapa Tanzania.

#WeAreBasketball