Baada ya kushiriki kwa mafanikio katika kambi ya Basketball Without Borders (BWB) na NBA Africa Game huko Afrika Kusini mbapo Mtanzania Jesca aling’ara kwa kuchaguliwa katika timu ya All Stars iliyocheza mchezo wa utangulizi kabla ya mchezo wa NBA.
Tanzania inapeleka tena vijana 13 wa chini ya miaka18 katika kambi ya Giants of Africa inayofanyika huko Nairobi, Kenya, kuanzia 15 hadi 20 August, 2018.

Msafara wa Tanzania unatuwakilisha Kenya ni kama ifuatavyo :
1. BAHATI MOSES MGUNDA (Kocha)
2. ATIKI ALLY ATIKI
3. OMAR MAALIM OMARI
4. QURAISH SLYVESTER MGANGA
5. HOSSAM RASHID KITILA
6. JOSEPHAT PETER SANKA
7. NOELA UWANDAMENO
8. JESCA NGISAISE ONG’ANYI
9. JUDITH PANTALEO
10. ANNA SAILEOU
11. CATHERINE LOISHIYE
12. MARY ROBERT
13. HUSNA MOHAMED
14. NEEMA JONAS

Kiongozi wa msafara huu huko Nairobi ni Kocha Bahati Mgunda.

Kambi hiyo inaendeshwa na Ndg. Maasai Ujiri ambaye ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Timu ya NBA ya Toronto Raptors ya Canada.

Rais wa TBF Ndg. Phares Magesa alipata nafasi ya mazungumzo na na Ndg. Ujiri walipokutana Afrika Kusini wakati wa NBA Africa Game na mipango na mazungumzo zaidi yanaendelea ili kambi hii kubwa ya Giants of Africa mwaka ujao na miaka mingine iweze kufanyika hapa Tanzania ili kushirikisha vijana wengi wa Kitanzania.

Pia Rais wa TBF alifanya mazungumzo na na Viongozi wa Timu za NBA za San Antonio Spurs na Indiana Pacers ambao nao wameonyesha nia ya timu zao kuja Tanzania mwaka ujao kuendesha Clinics za mafunzo kwa vijana na kushirikiana katika programs mbalimbali za maendeleo ya Kikapu Tanzania.

Pia Ndg. Magesa alifanya mazungumzo na Mchezaji gwiji wa kikapu Dikembe Mutombo ambaye nae ameonyesha nia ya kuja Tanzania kusaidia jitihada za kuendeleza kikapu nchini.

Pia tunapenda kuutarifu umma kuwa timu yetu ya Taifa ya U18 itashiriki Mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Mali ya 3×3 kwa wanaume mwezi Septemba mwaka huu.

Kuhusu FIBA Zone V Club Championship maandilizi yanaendelea vizuri, mshindano haya yatafanyika Tanzania kuanzia Septemba 30 hadi Octoba 7, 2018 ambapo timu 29 zimethibitisha kushiriki na pia timu 16 za Taifa kwa U23  zimethibitisha kushiriki mashindano ya 3×3 yatakayofanyika sambamba na Zone V Club Championship hapa nchini Tanzania.

Kwa sasa ligi za mikoa (RBA) zinaendelea na baadhi ya mikoa wamemaliza na baadae zitafuata na ligi za kanda na baadae ligi ya Taifa ya Kikapu (NBL) itafanyika.
Mashindano ya Kombe la Taifa (Taifa Cup 2018) yatafanyika mkoani Simiyu mwezi Novemba na matukio mengine yatakayofanyika mwaka huu ni Intercities Dodoma, Nyerere International Memorial Cup Musoma, Kilimanjaro Cup Arusha na mwisho wa mwaka mwezi Desemba tutakuwa na tamasha kubwa la wanakikapu wote Tanzania ( Basketball Gala & Hall of Fame) ambapo tutatoa tuzo kwa wadau wote wa kikapu walio hai na waliotangulia mbele ya haki.

Tunaomba wadau wa maendeleo na wafadhili wa  ndani na nje mjitokeze kushirikiana na TBF kufadhili matukio hayo na kusaidia katika programu mbalimbali maendeleo ya mpira wa kikapu nchini.

Phares Magesa
Rais,
Tanzania Basketball Federation (TBF)